Hunywi maji yakapita
Mi nkiguna ushafika
Jina gani hujaniita baby
Ushauri hutaki kabisa
Eti uniache nna visa
Vya Firauni na Musa vingi
Nikilala naota kama unaniita
Nafumba macho navuta shuka
Naona napumbazika
Unishikapo ndipo hapo nafarijika
Mambo yako mahaba yako
Ndo maana natononoka weh
Wana wana wana wana
Pale tulipokutana
Mikono tukapeana
Macho yakatizamana
Wana wana wana wana
Pale tulipokutana
Namba kubadilishana
Nafsi kukubaliana aah
Nzi kidondani huvia
Wahenga walisema
Maradhi yaweza yasiwe na dawa
Kwa penzi yakapona
Rabii amenipa nusura
Jeuri sina tena
We ndo ganzi umenimaliza hasira
Siumwi wakisema
Nidekeze niliwaze
Washushuke wanyamaze
Nikinuna nibembeleze
Usinipepee nipulize
Watuone washituke
Roho zao ziwaume
Mi nipike ule chote
Unenepe upendeze
Wana wana wana wana
Pale tulipokutana
Mikono tukapeana
Macho yakatizamana
Wana wana wana wana
Pale tulipokutana
Namba kubadilishana
Nafsi kukubaliana aah mmh
Ukitaka uniweze nibebe wewe
Ukipenda unibimbe unikumbatie
Hata watu watuone wakahadithie
Nitambulishe niringe niwavimbie
Ukitaka uniweze nibebe wewe
Ukipenda unibimbe unikumbatie
Hata Lizer atuone akahadithie
Nitambulishe nitambe niwavimbie (Wasafi)